Habari

Uchaguzi wa rais wafanyika Guinea

Raia wa Guinea wamepiga kura hapo jana siku ya Jumapili kumchagua rais, katika uchaguzi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali kati ya rais wa sasa Alpha Conde na mpinzani wake mkuu Cellou Dalein Diallo.

Uchaguzi huo unajiri mnamo wakati kumekuwa na maandamano ambayo wakati mwingine yalikumbwa na vurugu dhidi ya serikali kwa wiki kadhaa.

Maandamano hayo yaliongozwa haswa na makundi ya vyama vya upinzani, hali ambayo imesababisha maafisa wengi wa usalama kupelekwa katika maeneo mengi ya taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wagombea kumi na wawili wanawania urais lakini kinyang’anyiro kikali ni kati ya Rais Alpha Conde mwenye umri wa miaka 82 anayewania muhula wa tatu dhidi ya Cellou Dalein Diallo wa chama kikuu cha upinzani kiitwacho Umoja wa Vikosi vya Demokrasia (UFDG).

Wachambuzi wanabashiri kuwa Conde ambaye alishamshinda Diallo mara mbili katika chaguzi zilizopita, ataibuka mshindi tena kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano.´

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents