Habari

Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya usiku wa leo, vitu 7 vitakavyo badilika na vitakavyo salia

Baada kuzungumzwa na kukaliwa vikao mara kadhaa hatimaye siku ya Ijumaa Januari 31 saa tano kamili usiku, taifa la Uingereza linajiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Image result for brexit today"

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesifu kile amesema kuwa ni mwanzo mpya kwa Uingereza wakati ikijiandaa kuondoka Umoja wa Ulaya baada ya miaka 47.

Lakini moja kwa moja itaingia katika miezi 11 ya kipindi cha mpito, kwa hivyo ni nini kitakacho badilika?

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Wakati wa kipindi cha mpito Uingereza itaendelea kufuata sheria za EU na kutoa mchango wake wa kifedha kwa EU. Vitu vingine vitafanana na vingine vitakua tofauti.

1. Wabunge wa Uingereza katika bunge la Muungano wa Ulaya watapoteza viti vyaoNigel Farage akisherehekea celebrating with newly-elected Brexit Party MEPSChama cha Brexit cha Nigel Farage kilishinda viti vingi nchini Uingereza wakati wa uchaguzi wa Ulaya Mei 2019

Nigel Farage,Kiongozi wa chama cha Brexit na mwanaharakati mkuu anayeunga mkono kampeini ya Uingereza kujiondoa katika Muungano wa Ulaya atakuwa mmoja wa wabunge 73 wa Uingereza katika bunge la Ulaya watakayepoteza viti vyao moja kwa moja.

Hii ni kwasababu Brexit ikifanyika Uingereza italazimika kujiondoa katika taasisi za kisiasa za EU na mashirika yake.

Kando na kwamba Uingereza itafuta sheria ya Uingereza katika kipindi cha mpito, Mahaka ya Haki ya Ulaya – itaamua jinsi sheria za EU zitakavyotekelezwa – itaendelea kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu mzozo wa kisheria.

2. Hakuna tena kuhudhuria makongamano ya EU

Waziri mkuu wa Ungereza Boris Johnson atapewa mualiko maalum endapo atataka kuungana na viongozi wengine katika kongamano la baraza Ulaya siku zijazo.

Mawaziri wa Uingewre pia hawatahudhuria mikutano ya mara kwa mara ya EU ambayo inaamua maswala kadhaa muhimu

3. Tutasikia mengi kuhusu biashara

Uingereza itaweza kuanza mazungumzo ya kibiashara na nchi duniani kuhusu kuweka taratibu mpya za kununua na kuuza bidhaa na huduma.

Haikuwa ikiruhusiwa kufanya mazungumzo na nchi kama Marekani na Australia wakati ikiwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Kambi inayounga mkono kujitoa kwa Uingereza inasema kuwa itakuwa na uhuru wa kuweka sera zake za kibiashara kwa ajili ya kuinua uchumi wake.

Kuna mengine mengi ya kujadiliana na EU. Kwa kukubaliana kuwa makubaliano ya kibiashara kati ya Uingereza na EU ni muhimu, hivyo gharama za ziada kwa bidhaa na vikwazo vingine vya kibiashara havihitajiki pale kipindi cha mpito kitakapokamilika.

Ikiwa itafikia makubaliano ya kibiasha, hawataweza kuanza mpaka kipindi cha mpito kitakapokamilika.

4. Pasipoti ya Uingereza itabadilishwa rangiPasipoti za Uingereza

Pasipoti za Uingereza

Pasi za kusafiria za rangi ya bluu zitarejea, zaidi ya miaka 30 baada ya kubadilishwa na za sasa.

Akitangaza mabadiliko hayo mwaka 2017, waziri wa Uhamiaji wa, Brandon Lewis, alisifia kurejea kwa pasipoti ya kipekee ” za kale” za rangi ya bluu-na-dhahabu, ambazo zilitumika mwaka 1921.

5. Sarafu ya BrexitSajid Javid akiwa na sarafu ya mpya ya pauniSarafu hii ilibadilishwa baada ya Brexit kuchelewa

Karibu sarafu milioni 50 zilizo na alama ya tarehe “31 January” na iliyoandikwa: “Amani, Mafanikio,Urafiki na mataifa yote”, itaanza kutumika Ijumaa.

Sarafu hizo zimepokelewa kwa hisia mseto, huku wafuasi wanaotaka kubaki wakisema hawaikubali.

Serikali ilikuwa imepanga kuzindua sarafu hiyo Oktoba 31, tarehe ya awali iliyowekwa kwa ajiloi ya Brexit.

Hata hivyo sarafu hizo ziliyeyushwa na kuundwa tena baada ya muda wa mwisho kurefushwa.

6. Idara ya Uingereza ya Brexit kufungwa

Jopo la mashauriano ya Uingereza na Muungano wa EU ambalo limekuwa likiongoza mchakato wa Brexit litavunjwa.

Idara inayoendesha mchakato wa Uingereza kujiondoa Muungano wa Ulaya iliundwa na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Theresa May, mwaka 2016.

Kwa mazungumzo yatayofuata, timu ya mashauriano ya Uingereza itakuwa na makao yake Downing Street.

7. Ujerumani haitakuwa ikiwarudishawahalifu Uingereza

Haitawezekana kuwarejesha Uingereza watu wanaoshukiwa kuwa wahalifu waliiotorokea Ujerumani.

Katiba ya Ujerumani hairuhusu raia wake kushtakiwa katika nchini nyingine isipokuwa mataifa ya Muungano wa EU.

“Hatua hii haiwezi kufanyika tena baada ya Uingereza kujiondoa katika Muungano wa EU,” Msemaji wa Wizara ya Haki ya Ujerumani aliambia BBC.

Haijabainika kama udhibiti huo utahusisha nchi zingine za muungano huo. Slovenia, kwa mfano, inasema hali hiyo ni yakuchanganya, Lakini Tume ya Ulaya haikuweza kutoa tamko lolote kuhusu suala hilo.

Ofisi ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Uingereza inasema waranti ya kukamtwa ya Ulaya itaendelea kuzingatiwa katika kipindi cha mpito. (Hii inamanisha Ujerumani itaweza kuwarudisha nyumbani watu ambao si raia wake.)

Hatahivyo, imeongeza kuwa sheria ya nchi hiyo inawazuia kuwarudisha wahalifu Uingereza “Itarajiwa kumshitaki au kumhukumu mtu husika”.

Vitu saba ambavyo havitabadilika

Kwasababu kipindi cha mpito kinaanza mara tu baada ya Brexit, vitu vingi vitasalia kama kawaida- hadi tarehe 31 mwezi Disemba 2020:

1. UsafiriRaia wa Uingereza watahudumiwa sawa na raia wa mataifa ya Muungano EU katika kipindi cha mpitoRaia wa Uingereza watahudumiwa sawa na raia wa mataifa ya Muungano EU katika kipindi cha mpito

Ndege, boti na treni zitaendelea kuhudumu kama kawaida.

Linapokuja suala la udhibiti wa pasipoti, katika kipindi cha mpito, raia wa Uingereza wataruhusiwa kupanga foleni katika eneo lililotengewa raia wa mataifa ya Muungano wa EU wanaowasili tu/

2. Leseni ya kuendesha gari na pasipoti za wanyama :

Bora ziwe halali zitaendelea kutumika

3. Kadi ya Bima ya Afya ya Ulaya(EHIC)Kadi maalum ya bima ya afya kwa raia wa Uingereza zinaweza kutumika katika mataifa ya EUkatika kipindi cha mpitoKadi maalum ya bima ya afya kwa raia wa Uingereza zinaweza kutumika katika mataifa ya EUkatika kipindi cha mpito

Kuna kadi zinazotolewa na serikali kwa raia wa Uingereza ili wapate huduma za matibabu wakiwa wagonjwa au wakipata ajali.

Kadi hizo zinaweza kutumiwa katika mataifa wanachama wa Muungano wa EU country (pamoja na Uswizi, Norway, Iceland naLiechtenstein) zitaendelea kutumiwa katika kipindi cha mpito

4. Kuishi na kufanya kazi Uingereza

Uhuru wa kusafiri utaendelea kuzingatiwa katika kipindi cha mpito, kwahivyo raia wa Ungereza wataweza kuishi nchini humo na kufanya kazi EU kama wanavyofanya sasa.

Raia wa mataifa ya EU wanaotakakuisha katika nchi zao na kufanya kazi Uingereza pia hawatakabiliwa na vikwazo vya usafiri katika kipindi cha mpito.

5. Malipo ya uzeeni

Raia wa Uingereza wanaoishi katika mataifa wanachama wa Muungano wa Ulaya wataendelea kupokea malipo yao ya uzeeni na pia nyungeza yao ya kila mwaka.

6. Kuchangia bajeti

Uingereza itaendelea kuchangia bajeti ya EU wakati wa kipindi cha mpito. Hii inamaanisha mpango wa sasa, unaofadhiliwa na misaada ya EU, itaendelea kufadhiliwa.

7. Biashara

Biashara kati ya Uingereza na Muungano wa Ulaya itaendelea bila malipo yoyote ya ziada au kubuniwa kwa sheria mpya za forodhani.

Uingereza itaondoka katika Umoja wa Ulaya hii leo Ijumaa Januari 31 saa tano kamili usiku, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu baada ya kupigwa kura ya maoni mwaka wa 2016 ya kujiondoa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents