Michezo

Van Gaal: Najua mashabiki wa Man United hawafurahii mbinu zangu

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kuwa anatambua mashabiki wa klabu hiyo hawafurahii mbinu zake anazotumia.

Louis van Gaal

Hata hivyo Van Gaal alisema kuwa ushindi wao dhidi ya CSKA Moscow ulileta tabasamu Old Trafford. Baada ya uamuzi wa kocha huyo kumuondoa Anthoy Martial na badala yake kuingia Fellaini mechi ikiwa 0-0 alishtumiwa vikali huku mashabiki wakionyesha hisia zao kwa kumzomea.

Rooney aliipa United goli la ushindi kunako dakika ya 79.

“Mimi si kiziwi. Naelewa maoni ya mashabiki lakini mwishowe watafurahia,” alijitetea Van Gaal.

Bao la Rooney ambalo lilikuwa goli lake la 237 katika timu hiyo na kumweka katika nafasi ya pili pamoja na Denis Law kwenye orodha ya wafungaji bora wa United, lilikuwa la kwanza la klabu hiyo baada ya muda wa dakika 404.

Man United iliandikisha matokeo ya kutofungana kwenye mechi zake dhidi ya Manchester City, Middlesbrough na Crystal Palace.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents