Burudani

Vanessa Mdee: BET Awards si za Waafrika, ni za Wamarekani

Vanessa Mdee amesema anawashangaa wasanii wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wanaolalamika kuwaona wasanii wao wakipewa tuzo kabla ya show ya BET Awards.

Vanessa Mdee

Vanessa Mdee ambaye ni mmoja wa majaji wa tuzo hizo, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa BET wanashindwa kuonesha jinsi wasanii wa Afrika wanavyokabidhiwa tuzo kutokana na sababu za kibiashara na wadhamini.

“Unajua watu wanasahau kama zile tuzo sio za waafrika, it’s for African American,” amesema Vanessa. “Halafu ujue wale sio kama Kili, labda Kili wanapewa three hours halafu wanaongezewa kama nusu saa au dakika 15 wakiwa wanaonyesha kwenye TV. Wale two hours it’s two hours, ikizidi inakatwa, so lazima wavute watu ambao wataongeza viewership nyingi,” ameongeza.

“Marekani network zinalipwa kwa viewership, ndio maana unaambiwa rate ya show fulani ni kubwa, wana-monitor watu wangapi wanatazama, wanaget more money kupitia watu wanaowatazama. Kwahiyo wanajaribu kuvuta Wamarekani zaidi. Sasa kitendo cha msanii wa Afrika, Marekani anawajua waafrika? Hawajui, so tukilalamika tunakosea, kwa sababu hiyo tuzo sio za kwetu. Ndio tunataka na sisi tuonekane but it’s not our show na huwaingizii hela na mpaka tufikie hapo tushukuru hata wametupa hicho kipengele.”

“Ukiaangalia hata Chris Brown tuzo yake haikugawiwa pale kwenye stage, ni kwamba alishinda viewerS choice award ndIO akaenda akapokea viewers na ile nyingine. Za Beyonce uliona hata mtu mmoja ameenda kupokea pale kwenye stage? No, hata za kwao ziligawiwa red carpet. Kuna tuzo nyingi ambazo zinagawiwa mwanzoni,” alisisitiza Vanessa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents