Mitindo

Viatu chakavu vyauzwa kwa mamilioni ya dola

Jumba linalohusika na mitindo ya kifahari Balenciaga limeingiza sokoni aina mpya ya viatu vilivyotengenezwa katika muonekano wa uchakavu na hivyo kuzua gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii duniani.

Picha za viatu hivyo zilizopigwa na mpiga picha maarufu, Leopold Duchemin kwa ajili ya chapa hiyo mpya za viatu venyemuonekano wa uchakavu imekuwa gumzo tangu uzinduzi wake ulipofanyika siku ya Jumatatu.

 

Kwa mujibu wa jumba hilo la mitindo, ni pea 100 pekee za sneaker ambazo zimezalishwa na kuweza kupatikana kwa ghharama ya dola milioni 1,850 ambazo ni kama Tsh milioni 4 na laki 3.

Wakati matoleo mengine yatapatikana kupitia tovuti ya Balenciaga kwa dola 495, dola 625, kulingana na mtindo maalum ambapo ni sawa na zaidi ya  Tsh milioni 1.1 na zaidi ya shilingi milioni 1.4 kwa jozi moja.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents