Habari

Video: Chadema waeleza sababu za Lissu kutibiwa Nairobi

Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vincent Mashinji ameeleza sababu za kumpeleka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupatiwa matibabu mjini Nairobi nchini Kenya.

Dkt. Mashinji amesema hawana wasiwasi na madaktari hapa nchini kwa sababu wanajua madaktari wote wanafuata maadili ila wameona kuwa ‘stress’ za hilo shambulio kwa mtu lazima litamtisha na kumuweka kwenye mazingira ambayo atakuwa na uhuru na uponaji wea haraka kutokana na hali ya shambulio lenyewe lilivyotokea.

“Baada ya kuangali hali ya tukio lenyewe na nikatoa shukrani za dhati kwa madaktari wote nchini kama wezangu na hatuna wasiwasi na madaktari kwasababu tunajua wote wana maadili hilo sina wasiwasi nalo na ndio maana hata alivyoingia theathre alirudi salama na hata kama wakati wakusafiri walimuandaa vizuri na akasafiri salama,” amesema Katibu huyo.

“Kimsingi katika mafunzo ya udaktari ambayo wengine kwa bahati nzuri tume bahatika kuyaona cha kwanza katika maisha yako ni kulinda afya kwa hiyo hatuna mashaka na madaktari na wasaidizi wote manesi na wataalamu wa maabara katika kumuhudumia lakini pia tukumbuke hospitali ni mazingira kunaweza kukaja na watu mbalimbali wakaja kukusalimia. Kuna wema na ambao sio wema hata kwa maisha ya kawaida yawezekana huko vitu kama hivi vinatokea,” ameongeza.

“Kwa hiyo tukaona jambo jema na stress za hilo shambulio kwa mtu lazima litamtisha tutamuweka kwenye mazingira ambayo atakuwa na uhuru na uponyaji kwa sababu ile hali ya shambulio kwa mtu kazima litamtisha. Kwa hiyo tukamuweka kwenye mazingira ambayo atakuwa huru na amani hata uponyaji wa mwili una kwenda haraka. Gharama zitagharamiwa na chama chetu, kipo tayari na kimeshajipanga kuhakikisha kwamba anapata matibabu anayostahili, najua wote mnajua kazi anayoifanya Mhe. Lissu katika chama chetu kwa hiyo sidhani kama kuna mashaka ya sisi kugharamia,.”

“Ule mfumo wa matibabu wa Bunge hakwenda na mfumo ambao sisi hatukupendelea mgonjwa wetu apate kwa sababu wao walisema lazima aje kwanza Dar es Salaam na akishafika na wao sasa wataamua kwamba aende nje au laa, lakini kimsingi nilivyoeleza ili nae uponyaji wake uwe wa haraka katika mazingira yale tumekaa na wataalamu wetu tukaona ni vyema akaenda kutibiwa sehemu nyingine ambapo hata akiwa amesinzia hatakuwa na wasiwasi labda jamaa wanakuja tena kwa sababu navyo hivi vitu ni sychological,” amesisitiza.

Na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents