Habari

Video: Nape aeleza kwanini Dr Kikwete hakutengeneza uadui na wapinzani

Mbunge wa jimbo la Mtama kupitia tiketi ya CCM, Nape Nnauye amefafanua kauli yake ya kuiunga mkono kauli ya Rais mstaafu, Dr Jakaya Kikwete na kuwataka viongozi waafrika waache kuwachukulia wapinzani wa vyama vya siasa kama maaduzi zao.

Akiongea katika mahojiano maalumu na Bongo5 wiki hii mkoani Dodoma, Nape amesema siasa isiwafanye watu wakaanza kuchukiana na kujengeana chiki.

“Nilikomenti kupitia mitandao ya kijamii, nilisema mimi namuunga mkono Dr Jakaya. Wapinzani sio maadui, mimi nakaa nao napika nao chakula tunakula. Upinzani sio uadui, ni wadau katika kuendesha nchi, ndio maana mimi ishu ya Lissu nimepiga naye picha muda mchache kabla ya kupatwa na tukio, wapinzani wote mimi ni rafiki zangu na katika watu ambao wamefanya siasa za kupambana mimi ni mmoja wapo,” alisema Nape.

Aliongeza, “Wapinzani tuwachukulie kama ni washirika wetu, hakuna siku watatuunga mkono, lakini watatukosoa na tukiweka dhana hiyo hakuna siku tutawekeana vinyongo, halafu wakati mwingine sisi tunagombana wao wakubwa wanakaa meza moja wanakunywa chai, isifike mahali tukawekeana vinyongo tukataka kutoana roho, kwahiyo kimsingi namuunga mkono Dr Kikwete na yeye aliendesha nchi kwa ustarabu huo, anakunywa nao chai, kwanini hakuwachukulia kama maadui. Yapo mambo Kikwete aliyafanya wakati wake hata sisi wakati mwingine ndani ya CCM tulikuwa tunachukia, unakuta mahali mmembana mtu halafu yeye anafika anasema muacheni, leo tunasema tulikuwa tunasikitika lakini nadhani alikuwa anafanya sawa sio maadui zetu hawa,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents