Habari

Video: Rais Magufuli awakingia kifua wamachinga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Naibu Waziri TAMISEMI, Suleman Jafo na Katibu Mkuu (TAMISEMI), Mussa Lyombe kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo “Machinga” katika Jiji la Mwanza mpaka mamlaka husika itakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa.

2

Rais Magufuli ametoa agizo hilo Ikulu jijini Dar es Salaam huku akisema kuwa kiongozi ambaye hatatii agizo hilo aachie ngazi mara moja.

“Kumekuwa na tabia ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuwafukuza wamachinga bila utaratibu wowote, na wakati mwingine wanawapeleka maeneo ya mbali, ambapo hayafai hata kufanya biashara. Hili jambo sio sawa hata kidogo,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameagiza wamachinga ambao hawajatengewa maeneo yao warudi katika maeneo hayo waliyokuwa wakifanyia kazi mpaka pale watakapopangiwa mengine.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents