Bongo5 Exclusives

Video: Rick Ross akiwasili Hyatt Hotel, Director wa video zake aongea!!

Haikuwa rahisi kupata nafasi ya kuchukua picha za Rick Ross kutokana na ulinzi mkali lakini Bongo5 ilifanikiwa kupata kipande hiki kinachomuonesha Rick Ross akiwasili katika hoteli ya Hyatt akitokea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere.

Mwishoni mwa video hii utawashuhudia
akinadada walioanza kupiga kelele za furaha baada ya kumshuhudia hitmaker huyo wa ‘Aston Martin Music’ karibu yao.

Wakati huo tulipata fursa ya kuzungumza na muongozaji na mtayarishaji wa video za Rick Ross na wasanii wengine wa Maybach Music, Spiff TV aliyeambatana na rapper nchini Tanzania.

http://www.youtube.com/watch?v=4E7QJFc917M&feature=youtu.be

Kwenye interview hii Spiff TV anasikika akisema kuwa amefanya kazi na Rick Ross kwa muda mrefu na amekuwa akifanya video za wasanii wa MMG wakiwemo Meek Mill na wasanii wengine kama Drake, Waka Flocka, Diddy na wengine.

Mwanzoni anasikika akisema kuwa amefurahi kuja Tanzania nchi nzuri na atafurahia kuona simba.

Anasema video mpya ambayo ameifanya ni ya DJ Khaled ya wimbo wake I Did It For My Dawgs aliowashirikisha Rick Ross, Meek Mill, French Montana na Jadakiss.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents