Michezo

Video: Sitaki kucheza mapambano ya ndani ya Tanzania – Cosmas Cheka

Bondia Mtanzania mwenyerekodi ya kuchukua ubingwa wa dunia nje ya nchi, Cosmas Cheka amesema mchezo wa ngumi umepoteza hadhi yake nchini hii ni kwa sababu ya vyama vinavyosimamia mchezo huo kuwa na migogoro ya mara kwa mara.

Cheka ambaye ni mdogo wake na bingwa mwingine wa dunia, Francis Cheka ameyasema hayo kupitia Bongo5.

“Ngumi ni biashara ‘boxer’ na mapromota wapo katika biashara pamoja na wandaaji wa ngumi, matatizo yanayotokea katika vyama vinavyosimamia mchezo huu hapa nchini ndiyo yanayochangia mchezo huu kutoendelea na kufanya mabondia waonekana wahuni na kukosa wadhamini”.

“Mimi ni ‘boxer’ na kazi yangu ngumi hivyo najua kitugani nafanya, nimeshawaambia sitaki kucheza tena Tanzania kwa sababu tunarudiana vilevile hakuna tunachojifunza zaidi ya kuumizana tu hivyo wakitaka nicheze wanitafutie mpiganaji kutoka nje ya nchi”. Alisema Cosmas

Aliongeza kwa kusema, “Tanzania mchezo wa ngumi unadharaulika sana na ndiyo maana wachezaji ngumi wengi ni maskini licha yakuwa ni mchezo unauoongoza kwa kuleta mataji mengi zaidi kutoka nje ya nchi”.

Licha ya kuingia kwenye rekodi ya mabondia waliowahi kubeba ubingwa wa dunia nje ya ardhi ya Tanzania pia yupo kaka yake Frances Cheka ameingia kwenye rekodi ya mmoja wa mabondia waliobeba ubingwa wa dunia wakiwa nje ya nchi.

Wengine waliowahi kubeba ubingwa wa dunia wakiwa nje ya ardhi ya Tanzania ni marehemu Magoma Shabani aliyebeba ubingwa wa dunia wa WBU nchini Italia, Rashid Matumla aliyebeba ubingwa wa dunia wa IBU nchini Afrika Kusini.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents