Siasa

Viongozi 17 wakiwemo Mawaziri nane Manaibu na katibu Mkuu kuapishwa leo Chamwino

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia leo kuwaapisha Katibu Mkuu Kiongozi, mawaziri wanane pamoja na manaibu waziri wanane aliowateua jana tarehe 31/03/2021 baada ya kufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.

Kushoto ni Waziri Mteule wa wa Nchi katika Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu na Kulia ni Waziri Mteule wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo

Uapisho huo utafanyika leo Ikulu ya Chamwino Dodoma majira ya saa tisa alasiri, ambapo Katibu Mkuu Kiongozi mteule Balozi Hussein Athuman Kattanga ataapishwa wa kwanza.

Mawaziri wateule watakaoapishwa leo ni Mhe. Ummy Mwalimu, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Mhe. Selemani Jafo, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mhe. Geofrey Mwambe, Balozi Liberata Mulamula na Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Kwa upande wa manaibu waziri watakaoapishwa ni, Mhe. William Ole Nasha, Mhe. Abdallah Ulega, Mhe. Mwita Waitara, Mhe. Pauline Gekul, Mhe. Hamad Masauni, Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk, Mhe. Mwanaidi Hamisi, na Mhe. Hamad Chande.

Aidha, wabunge watatu walioteuliwa jana wameshakula kiapo mbele ya bunge Dodoma, ambao ni Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Liberata Mulamula na Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents