Burudani

Viongozi wengi huvaa nguo za Born to Shine,ila naogopa kuwapost – B12

Wiki hii kwenye Supermega ya Kings FM tulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu baadhi ya viongozi na watoto wa viongozi nchini Marekani ambao wanaonekana wanavaa either nguo ama kofia ambazo ni brand zinazomilikiwa na wasanii nchini humo.

Swali likawa kwanini hapa Tanzania utamaduni wa viongozi na watoto mashuhuri wa viongozi hao wa kuvaa brand za wasanii ama watu maarufu haupo? Simu iliyopigwa studio na CEO wa Born to Shine ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds FM, B12, ikatoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya viongozi wanaomsupport kwenye brand yake.

“Tofauti ya Tanzania na nchi nyingine,nikimpost kiongozi wa CCM amevaa T-Shirt ya Born To Shine, maana yake watu wa vyama vingine watanichukia,” amesema Dozen.

“Nikipost mtu wa UKAWA, CCM watanimind kwa maana hiyo naamuaga kuachana nazo yAani wao huwa siwapost. Lakini watu wengine wa kawaida ambao ni wasanii huwa nawapost,” ameongeza.

Born to Shine ni moja ya brand za muda mrefu zinaendelea kuwepo sokoni bila kutetereka.

Na Prince Ramalove (Kings FM)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents