Vuvuzela kupigwa stop!

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Kombe la Dunia, Danny Jordaan jana alisema kwamba kuna uwezekano Vuvuzela zikapigwa marufuku. Malalamiko yamekuwa mengi kutoka kwa wadau mbali mbali, zikianza kwa wachezaji ambao wanasema kelekele zinazidi na wanashindwa kucheza, wakifwatia baadhi ya mashabiki ambao wanahofia kuhathiriwa kiafya kutokana na makelele kuzidi.

 

Pia zimekuwa kero kwa watanazaji wa TV na Redio ambao wanashindwa kusikika wanapofanya kazi zao. Captain ya timu ya Ufaransa, Patrice Evra amesema kwamba timu yake imepata tabu sana, wanashindwa kulala usiku kutokana na makelele ya vuvuzela, na pia hawasikilizani wanapokuwa wakicheza uwanjani.

“Ningependa tuimbe ama tushangilie kama kawaida” Jordaan amewaomba washabiki.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents