Tragedy

Shambulio la Westgate: Wabunge kuwahoji maofisa wa juu wa Usalama kuhusiana na kufeli kwa masuala ya kijasusi

Maofisa wa juu wa Kenya wanatarajiwa kuhojiwa na wabunge kuhusiana na kile kinachodaiwa kama kufeli kwa masuala ya kijasusi kufuatia shambulio baya la kigaidi kwenye jengo la Westgate lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 60.

article-2437201-184BF68D00000578-939_634x409

Mkuu wa kamati ya ulinzi ya bunge la Kenya anasema wananchi wanapaswa kujua ufa halisi wa mfumo wa usalama nchini humo. Kuna ripoti kuwa mamlaka ya ujasusi ya NIS ilitoa onyo kuhusiana na shambulio la kigaidi mwaka mmoja uliopita.

Vyanzo vya kiusalama vimeliambia shirika la habari la Uingereza, BBC kuwa wanamgambo wa Al-Shabaab walikodi duka kwenye jengo hilo wiki kadhaa kabla ya shambulio.

Maofisa wa usalama akiwemo mkuu wa kitengo cha ujasusi cha Kenya (NIS), Michael Gichangi – wanatarajiwa kuhojiwa leo na kamati ya ulinzi ya bunge. Kamati hiyo inataka pia jinsi mchakato wa operesheni ya uokozi ulivyokuwa kutokana na kuwepo mkanganyiko wa nani alikuwa msimamizi.

Magazeti ya Kenya yanadai kuwa NIS ilionya mwaka mmoja uliopita kuhusiana na uwepo wa wanamgambo wa al-Shabab jijini Nairobi waliokuwa wanapanga kufanya mashambulio ya kujitoa muhanga katika maeneo mbalimbali likiwemo eneo la manunuzi la Westgate.

Source: BBC News

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents