Habari

Wanasheria wamuunga mkono RC Makonda kuwasikiliza waliodhulumiwa

Dhamira njema ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuamua kuwasaidia wanyonge walioteseka na kunyanyasika muda mrefu baada ya kudhulumiwa Mali zao walizochuma kwa Jasho imewafanya Wanasheria kuguswa na kuamua kujitokeza kusaidia jitiada hizo ili kuhakikisha haki ya mnyonge inapatikana pasipo kuvunja Sheria.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi hao.

RC Makonda amesema idadi ya Wanasheria imeongezeka kutoka 160 hadi kufikia 246 siku ya leo ambapo ameshukuru Uongozi wa Shule ya Wanasheria kwa Vitendo (Law school), Mawakili wa kujitegemea pamoja na Chama cha Mawakili (TLS) kwa kumuunga mkono na kuwaomba wanasheria wengine kujitokeza kuwasaidia wananchi.

Aidha RC Makonda ameshukuru jopo la wanasheria wanaohudumu kwenye Zoezi hilo kwa umakini na huduma nzuri wanayotoa kwa wananchi waliojitokeza kitendo kinachowapa faraja wananchi ambao wametaabika kwa miaka mingi kutafuta haki yao.

RC Makonda amesema lengo lake ni kuhakikisha kila mwananchi aliefika na kupata namba anasikilizwa kwa umakini chini ya jopo la wanasheria makini wasiopungua Saba.

Baadhi ya wananchi akiwemo Mzee Paul Kiakaisho yeye anasema ameteseka kwa miaka Saba akitafuta haki baada ya kutapeliwa nyumba na alipowatafuta mawakili walimwambia ili waweze kumsimamia apate haki anapaswa kulipa million tano ambayo kwa Hali yake ngumu ya maisha Hakuwa na uwezo hivyo amemshukuru RC Makonda kutenga siku tano za kusikiliza Wananchi Bure.

Zoezi la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi waliodhulumiwa haki zao linaendelea hadi ijumaa ya February 02 likihusisha wenye malalamiko ya Kudhulumiwa Nyumba, Viwanja, Mirathi, Kazi, Magari,waliodhulumiwa kampuni zao,waliopata ulemavu makazini pasipo kulipwa,waliobakwa na kupoteza maisha pamoja na utapeli wa kukusanya Hati kama mkopeshaji kisha kuchukuwa mkopo Bank na kukimbia baadae Watu wanauziwa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents