HabariMichezo

Wanne Simba SC kuikosa Azam FC

Wakati Simba SC inajipanga kushuka uwanjani Benjamin Mkapa kuwakabili Wanalambalamba Azam FC, itakosa huduma ya wachezaji wake wanne kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Klabu ya Simba wachezaji hoa wanne ni Kanoute, ambaye anaugua tonsils (mafindofindo), Israel Patrick amepata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga.

Wengine ni Jimmyson Mwanuke ambye bado anendelea kuuguza majeraha na Mzamiru Yassin anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Hata hivyo Kanoute hali yake inazidi kuimarika na ameanza mazoezi ya Gym, wakati Israel Patrick huenda akawa nje ya uwanja kwa wiki mbili.

Imeandikwa na Hamza Fumo (Instagram @fumo255 )

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents