Bongo Movie

Wasionyonyesha watoto kuhofia maziwa kulala wafundwa na Ray Kigosi

Msanii wa filamu Bongo, Ray Kigosi ametoa somo zito kwa wadada wanaonyonyesha watoto.

Muigizaji huyo amesema amekuwa akipokea jumbe nyingi kutoka kwa watu mbali mbali zikimtaka kueleza siri ya mtoto wake na Chuchu Hansy, Jaden kukua haraka na kuonekana mchangamfu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray amekuwa na haya ya kusema; kuhusiana na hilo;

Unamkuta mdada kajifungua mtoto eti anaogopa kumnyonyesha mtoto wake kwa kipindi kirefu akiogopa  maziwa yake kuanguka bila kujua kama maziwa ya mama ni lishe bora ya mtoto kuliko vyakula vyote unavyovijua wewe.

Kumfanya mtoto kutoumwa mara kwa mara kumfanya mtoto awe mchangamfu muda wote coz maziwa ya mama ni kinga kubwa sana kwa mtoto kitaalamu hata kidini kama sijakosea wanakwambia mtoto lazima anyonye kwa muda wa miaka miwili, sasa je hao madada kwa kipini hiki wapo?.

Maana unamkuta madada kajifungua mtoto leo baada ya wiki utamkuta yupo disco anaruka majoka sasa hapo unategemea mtoto awe na afya gani ndio maana hata kwa madada wanaofanya kazi kipindi wajifunguapo utapata miezi mitatu ya kupumzika angalu basi mtoto apate malezi bora ya mama kitaalam wanaita (maternity leave) kama umeamua kuwa na mtoto jitahidi kumpa malezi yanayostahili kama mzazi.

Kwa kweli nimpongeze sana Chuchu kwani ni mwanamke wa tofauti sana maana mpaka sasa bado mtoto wetu ananyonya maziwa yake bila kuogopa wale kujali kama yataanguka na kizuri zaidi kaniambia mpaka ifike miaka miwili ndio mtoto atamuachisha kumnyonyesha.

January mwaka jana Ray Kigosi na mpenzi wake Chuchu Hansy walijaliwa mtoto wa kiume ambaye wamempatia jina la Jaden.

Soma Zaidi; Picha: Mpenzi wa Ray Kigosi, Chuchu Hans ajifungua mtoto wa kiume

Kwa sasa Jaden ni miongoni mwa watoto maarufu Bongo, ana followers 107k katika mtandao wa Instagram akiwafukuzia kina Tiffah, followers Milioni 1.6 na Nillan, followers 543k (wote wa Diamond, pia kuna Cookie wa Aunt Ezekiel na Mose Iyobo, followers 420k na wengineo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents