Habari

Watu 20 wafariki ‘Night Club’ nchini Afrika Kusini

Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza vifo vya karibu watu 21 vilivyotokea katika klabu moja ya usiku ya mji wa pwani wa East London mapema jana.

Maafisa wamesema wengi wa wahanga walikuwa watoto wa hadi umri wa miaka 13.

Haijabainika kilichosababisha vifo vya vijana hao, walioripotiwa kuwa walikuwa wamehudhuria hafla ya kusherehekea kumalizika kwa mtihani wa msimu wa baridi.

Gazeti la nchini humo la Daily Dispatch liliripoti kuwa miili ilikuwa imetapakaa kwenye meza na viti bila ya dalili za wazi za majeraha.

Msemaji wa wizara ya afya Siyanda Manana amesema kwa sasa hawawezi kuthibitisha chanzo cha kifo hadi watakapokamilisha upasuaji wa maiti haraka iwezekanavyo.

Rais Cryil Ramaphosa ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents