Habari

Waziri Mkuu ampa Mwakyembe siku 7 kujieleza juu ya hili

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ametoa muda wa wiki moja kwa waziri wa katiba na sheria Dr Haryson Mwakyembe kutoa maelezo kwa nini Tanzania haijakamilisha Mkataba wa Mawakili wa Afrika Mashariki kutambuana katika utendaji wao.

jn1-768x374
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Mwaka wa 21 wa Chama cha Wanasheria Afika ya Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ametoa agizo hilo Ijumaa hii wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli, katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa mwaka wa chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki kwenye kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Serikali zetu za Afrika Mashariki Tanzania,Kenya, Burundi na Rwanda zinaheshimu wanasheria zinathamini wanasheria lakini zinatambua kazi kubwa mnazofanya wanasheria katika kutafasiri mambo yanayogusa maendeleo katika nchi zetu. Nitumie nafasi hii kwa wanasheria zisaidieni nchi hizi ili ziepukane na umaskini uliokithiri na serikali zake zipate muda wa kushirikiana na watu wake, katika kufanya kazi ili wapate maendeleo,” alisema Majaliwa.

“Nimeshtushwa kidogo kusikia kwenye taarifa yenu kuwa mkataba huo uliolenga nchi zote za Afrika Mashariki hautaihusisha Tanzania kutokana na kutokukamilisha sehemu yao ya kuufanyia kazi, nitahitaji maelezo. Nitapenda kupata maoni yako wewe mwenyewe Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania kwa vile wewe ni Mwanasheria mwandamizi na siyo Mwanasheria wa Tanganyika Law Society peke yake kwa nini Tanzania haijakamilisha mkataba huu,” alihoji.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents