Siasa

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich akamatwa baada ya kujisalimisha kuhusu tuhuma za ufisadi

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich akamatwa baada ya kujisalimisha kuhusu tuhuma za ufisadi

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich amejisalimisha kwa maafisa wa upelelezi hii leo, muda mfupi baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini kuagizwa akamatwe.

Kwa mujibu wa Nairobi News, Waziri Rotich alipelekwa kwa gari hadi katika makao makuu ya idara ya upelelezi ambako anahojiwa kuhusu malipo yaliotolewa kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini.

Anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa.

Kwa mujibu wa BBC.Hapo awali, mkurugenzi wa mashtaka Kenya aliagiza kukamatwa kwa waziri wa fedha Henry Rotich na ashtakiwe kuhusu ufisadi

Mkurugenzi huyo wa mashtaka Noordin Haji amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kumshtaki waziri wa fedha Kenya Henry Rotich, na maafisa wengine wa serikali kuhusu kandarasi zilizotolewa kwa kampuni ya Italia kujenga mabwawa mawili.

Noordin Haji ameeleza kwamba watashtakiwa kwa “kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi” miongoni mwa mambo mengine.

Mashtaka hayo yanahusiana na ujenzi wa mabwawa mawili nchini uliogharimu fedha nyingi.

DPP NOORDIN HAJJIHaki miliki ya pichaKTN

Mnamo Machi Waziri Rotich alikana kupitia tangazo kubwa kwenye gazeti nchini kufanya makosa yoyote.

Kampuni hiyo ya Italia CMC de Ravenna pia imekana tuhuma hizo.

Umuhimu wa uadilifu kwa mujibu wa katiba

“Katiba yetu inasisitiza baadhi ya maadili yetu yakiwemo uadilifu… kuyatimiza hususan kwa walio uongozini…”

“Kutimizi maadili haya ni muhimu kwa uhai wetu…’ amefafanua mkurugenzi huyo wa mashtaka.

“Rushwa inatishia msingi wa taifa letu – ufisadi unatugawanya na kuangamiza utu..”

“Kila kesi inatuma ujumbe mzito kwa walio wafisadi … au kwa wanoavutiwa kuingia katika ufisadi… kwamba watashtakiwa…”

Haji ameeleza kwamba kashfa kuhusu ujenzi wa mabwawa hayo umewagharimu Wakenya walipoa kodi mabilioni ya fedha katika malipo yanayotiliwa shaka.

Maafisa wengine walioagizwa kukamatwana kushtakiwa ni pamoja na katibu mkuu katika wizara ya fedha Kamau Thugge, Dkt Susan Jemutai Koech kutoka wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki na mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya maendeoe ya Kerio Valley (KVDA) David Kimosop.

Taarifa kuhusu gharama ya ujenzi wa mabwawa hayo ziligubika mijadala katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini mnamo Machi mwaka huu.

Mamlaka ya Kerio Valley Development Authority (KVDA) ilitoka wazi na kujaribu kuzima tuhuma kwamba imeilipa kampuni ya hiyo ya Italia shilingi bilioni 21 za Kenya na kufafanua kwamba ni shilingi bilioni 7.6 pekee.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, KVDA ilisema mkandarasi huyo – CMC Di Ravenna – alilipwa kwa mafungu mawili kujenga mabwawa hayo ya Arror na Kimwarer katika kaunti ya Elgeyo Marakwet Kaskazini mwa Kenya.

Kulikuwa na kilio cha umma nchini Kenya kufuatia ripoti kwamba mabilioni ya fedha yalionuiwa kufadhili mradi wa bwawa la maji katika eneo la Bonde la ufa magharibi mwa Kenya zimetuhumiwa kufujwa.

Wakenya walijitosa katika mitandao ya kijamii kuelezea hasira na kuchoshwa kwa kile wanachotaja kuwa ni vitisho vya bure kwa viongozi wafisadi katika serikali.

Akizungumzia kuhusu uchunguzi kuhusu namna kandarasi za ujenzi wa mabwawa hayo zilizvyotolewa, Mkurugenzi wa mashtaka Kenya Noordin amesema:

“Imebainika kwamba namna mpango ulivyoidhinishwa, ulivyo patikana na malipo yalivyotolewa kwa mradi wa mabwawa hayo, umegubikwa kwa ukiukaji mkubwa wa sheria.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents