Burudani

Weusi wasema wametumia lugha ya kikubwa kwenye ‘Amsha Dude na Nicome’

Kundi la muziki wa hip hop Bongo, Weusi limesema kilichofanyika katika ngoma zao ‘‘Amsha Dude na Nicome’, ni sanaa/lugha ya kikubwa.

Rapper wa kundi hilo Joh Makini amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm walichofanya katika ngoma hizo mbili ni kucheza na maneno bila kukiuka maadili.

“Hiyo ni art, sisi tunatumia sanaa, naweza kuongea maneno ambayo kwa lugha nyingine usingeweza kuyatamka kwenye redio lakini kwa sababu natumia sanaa tunaweza jinsi ya kucheza na maneno kufikisha jumbe ambao tunautaka bila kuvunja sheria au kumkwaza mtu yeyote” amesema Joh Makini.

Amsha Dude na Nicome pamoja na Yakulevya ni ngoma ambazo kundi hilo wametoa kwa mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents