Habari
WHO imesema haiungi mkono baadhi ya nchi kuwaondoa wananchi wao China kisa Corona
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema WHO haiungi mkono baadhi ya Nchi kuwaondoa Wananchi wao China ili kuepuka maambukizi ya Virusi vya Corona.
“WHO ina imani China ina uwezo mkubwa wa kuzuia na kudhibiti maambukizi hayo” Taarifa hiyo imeeleza.
Kauli ya WHO inakuja kufuatia Japan na Marekani kuwaondoa Raia wao waliokuwa Wuhan eneo ambalo virusi hivyo vilianzia na Watu wengi kuathirika zaidi.
Idadi ya Watu waliofariki kwa Virusi vya Corona imefikia 132 China huku wagonjwa waliothibitishwa kuwa na Virusi hivyo wakifikia 5974.