Michezo

Yanga yaipeleka Bodi ya ligi FIFA na TAKUKURU, sakata la Kabwili lafika pabaya ”Tukusanye ushahidi”(+Video)

Klabu ya Yanga kupitia kwa Msemaji wa wake Hassan Bumbuli imeweka wazi ya kutoridhishwa na utendaji wa Bodi ya Ligi hasa kuzuia fedha zao zilizotoka kwa Mdhamini Mkuu wa Ligi Vodacom huku wakidai kutotendewa haki kupitia chombo hicho kila wanapopeleka malalamiko na kuonekan kuyapuuza na hivyo wanapeleka nakala za barua TFF, Baraza la Michezo, Waziri, Shirikisho la Mpira wa miguu duniani FIFA na TAKUKURU.

Bumbuli amegusia pia sakata la kipa wake Ramadhani Kabwili na kusema kuwa wamemuita mchezaji huyo na sasa wanatarajia kukusanya ushahidi ili jambo hilo kufikishwa sehemu husika.

”Hoja yetu sisi kama Yanga tunasema kwa nini tumepigwa faini ya juu kabisa wakati hatujasikilizwa, sisi kama klabu tunahisi hawajatutendea haki katika haya yote ambayo tumeyaeleza. Tumewaambia Bodi ya Ligi kwamba hatujarizika namna ligi inavyoendeshwa na pili wanavyoyachukulia kienyeji mambo tunayoyapeleka.” Yanga

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents