Burudani

Wizkid aahirisha tena kuachia album mpya mpaka mwakani (2016)!

Mashabiki wa Wizkid waliokuwa wakisubiri kwa hamu album mpya ya staa huyo ambayo ilipangwa kutoka Septemba, watalazimika kuvuta tena subira hadi mwakani 2016.

wizzy

Wizkid ametangaza kuahirisha kutoa album yake ya 3 mwezi huu (Septemba), baada ya kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya 2Face Idibia aliyefikisha miaka 40.

Amesema amegundua bado ana kazi kubwa anayotakiwa kuifanya kwenye muziki kutokana na alichojifunza kwa mkongwe 2 Face.

Hata hivyo ameahidi kutoa EP ya nyimbo 10 pamoja na video 10 mwezi October 2015.

Mpaka sasa Wizkid ameachia album 2, “Superstar” ya mwaka 2011 pamoja na “Ayo” ya mwkaa 2014.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents