Bongo Movie

Yanga Bongo Movie V Simba Bongo Movie

Simba_movie_Mpira

Timu ya wasanii wa filamu waliamua kujigawanya katika mafungu mawili, ya Simba na Yanga ilikuweza kukamilisha mazoezi ambayo ndani yake yalikuwa na kikombe. Lengo la mazoezi hayo ni  kujiandaa na kandanda ambalo watakuja kucheza na Wabunge siku ya jumamosi ijayo, huko Dodoma.


Katika mechi hiyo wadau wa Bongo MovieMama Rupia, na Mussa ambao walitoa mchango wao na kufikia zaidi ya milioni2, papo kwa  hapo kwaajili ya maandalizi mazima ya safari hiyo.

 

Katika mechi hiyo, timu ambayo wakereketwa wa Simba yaani Simba Bongo Movie, iliibuka na mabao mawili yaliyoingizwa nyavuni na Hassabi Kiduku, na bao la kufutia machozi lilifungwa na Vicent Kigosi maarufu kama Ray kwa mkwaju wa penati.

Yanga_Movie_Ray_Cluod

Ray na Cloud 112 wakisikiliza mawaidha ya kocha, baada ya kipindi cha kwanza kufungwa.

Yanga_Movie_Wema

Wema Sepetu akiwa amemkalia Jack Wplper, na pembeni yao ni Janert ‘Odama’ wakisikiliza maneno ya kocha

Yanga_Movie_Ray

Ray akipokea mkono kutoka kwa mgeni, baada ya kufungwa timu yao na kuwa washindi wa pili

Yanga_Movie_Kanumba

Steven Kanumba yeye anasema alijua kama watafungwa, hivyo aliamua kujificha nyuma ya mti na kuangalia mpira kwa kuchungulia, huku akijikinga na jua.

Simba_Movie_kikao

Baada ya mpira kuisha, wasanii wote walikusanyaika sehemu moja, kwaajili ya kusikiliza maelezo kutoka kwa viongozi wa filamu Tanzania maarufu kama Bongo Movie, Chiki, Steven Nyerere, Cloud na wengine kwaajili ya maandalizi ya safari.

Sima_Movie_Kate

Hapa mshabiki wa kweli na kiongozi na mdau wa Yanga Sport Club, Kate akiishabikia timu yake ya Yanga Bongo Movie, huku akipuliziwa Vuvuzela.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents