Michezo

Yanga Sc: Iwe jua iwe mvua ushindi leo lazima

Klabu ya soka ya Dar es salaam young Africa hii leo inatupa tena karata yake katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania, dhidi ya klabu ya Tanzania Prison mchezo utakao kuwa wa vuta ni kuvute kwa pande zote mbili hasa kutokana na umuhimu wa kila klabu kupata matoke chanya katika mchezo huo .

Yanga ambayo ipo katika mbio za kutafuta ubingwa wa ligi kuu kwa udi na uvumba kwa mwaka huu ili iweze kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika hapo mwakani, ili hali kwa upande wa klabu ya Prison inapata takribani michezo zaidi ya 6 haija pata matokeo mazuri pindi inapokutana na Mabingwa wa tetezi wa ligi klabu ya Yanga na hivyo wanahitaji kudhihirisha ubora wao na kufuta uteja uliojitokeza katika michezo iliyopta.

Katika mchezo wa mwisho ambapo timu hizi zilikutana ni katika michuano ya kombe la shirikisho ama, Azam Sports Federation Cup mchezo uliopigwa April 22, 2017 na Yanga walitoka na ushindi wa mabao 3 kwa 0 dhidi ya Prison.

Mchezo wa leo Yanga wanaingia uwanjani wakiwa na njaa ya matokeo ambayo yata wafanya wa wafikie watani zao wa jadi Simba Sc kwa idadi ya alama na Yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya wastani wa magoli. Yanga ina alama 56 ikiwa imecheza mechi 25 alama tatu nyuma ya Simba Sc ambayo imecheza mechi 27 hadi sasa ikiwa na alama 59.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents