Michezo

Zawadi za ligi kuu ya Vodacom kutolewa mwezi ujao

Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Yanga, Azam FC,Simba na Prison, pamoja na mchezaji bora,mfungaji bora wa ligi na kocha bora wa msimu huu ulioisha wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara, watakabidhiwa zawadi zao mapema mwezi ujao na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi hiyo.

001.PR

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa ucheleweshaji wa kutoa zawadi hizo baada ya kumalizika msimu wa ligi hiyo mwezi uliopita umetokana na baadhi ya timu zinazoshiriki kwenye mechi za mashindano ya kimataifa kama vile mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika na kuingia kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

“Tunaomba radhi kwa timu husika,wachezaji na wadau wa soka kwa zoezi hili kuchelewa ila tunawahakikishia kuwa zawadi ziko tayari na zitakabidhiwa mapema mwezi ujao,”alisema Nkurlu.

Pia alishukuru wadau wote waliofanikisha ligi hiyo hadi kufikia mwisho ambapo timu yanga ya jijini Dar es Salaam iliibuka tena bingwa kwa mwaka huu “Licha ya changamoto zinazoendeleza kujitokeza katika ligi yapo mafanikio makubwa na ligi hii inazidi kuwa na msisimko mkubwa nchini tunawashukuru wadau wote na tuna imani kuwa itazidi kuwa bora katika siku za usoni”

Alisema kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutoa udhamini wa ligi hii hata katika msimu ujao kwa mujibu wa mkataba wake na TFF na aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi hii ikiwemo kuwawezesha wachezaji kunufaika zaidi katika ushiriki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents