Habari

Agnes na Melisa ndio Watanzania waliokamatwa na ‘UNGA’ Afrika Kusini wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 6!

Wanawake wawili waliokamatwa katika uwanja wa ndege OR Tambo Afrika Kusini wakitokea Tanzania Ijumaa (July 6) wakidaiwa kuwa na madawa ya kulevya takribani kilo 150, wamefahamika kwa majina na ni raia wa Tanzania.

Nzowa(1)
Kamanda Godfrey Nzowa

Akizungumza na gazeti la NIPASHE jana (July 8), Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (25) ambaye alisema amezaliwa mwaka 1988 na Melisa Edward (24) ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Nzowa ameendelea kusema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini wapi zilikotokea dawa hizo, na pia linawasaka wamiliki wa dawa hizo.

Ijumaa (July 5), shirika la habari la Afrika Kusini (SABC) liliripoti taarifa juu ya kukamatwa kwa wanawake wawili (ambao hawakutajwa majina wala uraia) waliowasili na ndege kutoka Tanzania, wakiwa na mabegi 6 yaliyojaa madawa aina ya Crystal Methamphetamine maarufu kama ‘tik’ nchini humo, yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.

“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa. Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema msemaji wa mamlaka ya mapato ya Afrika Kusini (SARS) Marika Muller.

Tokea taarifa hizi kuripotiwa wikendi iliyopita Kumekuwa na uvumi ulioenea mitaani kwamba kuna uwezekano kuwa Agnes aliyetajwa na kamanda Nzowa ni yule model maarufu ambaye ameshatokea katika video nyingi za muziki hapa bongo (Kama Masogange) maarufu kama Agnes masogange (hatujathibitisha hilo).

agnesss
Agnes Masogange

Baadhi ya sababu zinazofanya watu wahusishe majina yaliyotajwa pamoja na uvumi uliopo ni kuwa jina analotumia Agnes Masogange katika mtandao wa kijamii ni (AGNESS GERLAD) na umri alioandika katika akaunti hiyo ni (9 September 1988) sawa na taarifa zilizotolewa na Kamanda Nzowa.

Melis
Mellis Edward

Na kitu kingine inahisiwa kuwa mwanamke wa pili aliyetajwa na Kamanda Nzowa kwa jina la “Melisa Edward” ‘inahisiwa’ kuwa ni mdogo wake na Agnes ambaye katika akaunti ya facebook anatumia jina la (MELLIS EDWARD) na Agnes amemuweka katika orodha ya family kama ‘sister’ katika akaunti yake ya Facebook.

Kuhusishwa kwa majina yaliyotajwa na uvumi ulioenea mtaani ni kutokana na kufanana kwa majina yaliyohusishwa katika uvumi huo pamoja na majina yaliyotajwa na kamanda Nzowa (sisi hatujathibitisha uhusiano huo hivyo bado ni fununu).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents