Habari

Hatimaye ROBA wa KALAMASHAKA azungumza baada ya taarifa za kuonekana akiuza KARANGA mitaa ya Nairobi kusambaa!

Siku chache zilizopita habari kuhusu member mmoja wa kundi kongwe la hip hop KALAMASHAKA zilienea katika mitandao ya Kenya zikisema kuwa inasemekana rapper huyo amegeuka kuwa omba omba na kaathirika na matumizi ya madawa ya kulevya, lakini lililobeba vichwa vingi vya habari yake ni kageuka kuwa muuza karanga katika mitaa ya Umoja, jijini Nairobi.

Roba

Kwa mujibu wa vyanzo ambavyo havikutaja jina la member katika habari hiyo ya awali, vilisema member huyo alionekana katika mitaa hiyo akiomba pombe katika club za usiku pamoja na kugongea sigara.

Baada ya habari hiyo kuandikwa member mmoja wa K-Shaka aitwaye Roba baada ya kuhisi kuwa ni yeye ndio amezungumziwa, ameamua kuvunja ukimya na kuongea kupitia ukurasa wake wa facebook.

Roba aliandika “So, Naskia na uza Njugu siku hizi Umoja, Umoja ni Mtaa yangu, I was gonna say isn’t me, but then wacha wajibambe”.

Kuuza karanga sio tatizo hata kidogo sababu ni biashara kama biashara nyingine, lakini kuuza karanga hizo hizo kwa msanii wa kundi kongwe na lenye historia ya mchango mkubwa katika muziki wa hip hop Kenya kama Kalamashaka, ndicho kinachosababisha watu wengi kushtushwa na hatua hiyo sababu ni ishara za kuanguka kimuziki na kiuchumi kwa kundi hilo.

Source: Kenyan Post

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents