Uncategorized

Kamishna aliyepewa adhabu na TFF kwenye mechi ya Yanga na Coast Union Afariki dunia, Rais Wallace Karia atuma salamu za rambirambi

Mwamuzi Mstaafu mwenye beji ya FIFA Charles Mchau amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi.

Taarifa za awali zinaeleza Mchau ambaye pia amekuwa akilitumikia Shirikisho Ia soka Tanzania (TFF), amefariki dunia baada ya kufikishwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC na kufanyiwa upasuaji wa vidonda vya Tumbo.

Mwamuzi Charles Mchau ni miongoni mwa waliofikwa na rungu la adhabu la TFF katika mchezo namba 239 kati ya timu ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya Yanga,mchezo uliopigwa Februari 3 2019 na kumalizika kwa sare ya bao 1 kwa 1.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga, Mchau aliyekua kamishna wa mechi na Mwamuzi Nassoro Mwinchui walitangazwa kufungiwa kwa miezi mitatu kila mmoja kutokana na taarifa zao kuwa na upungufu, na kushindwa kuumudu mchezo huo. 
Adhabu dhidi yao ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuukuhusu Udhibiti kwa Makamishna, na Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa waamuzi wa ligi.

Kwa upande wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kupitia kwa rais wake Wallace Karia wamepokea kwa maskitiko taarifa za kifo hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents