Tupo Nawe

Madrid ya Zidane na ‘Plan A’ yake, Hazard, Pogba, Mbappe na Mane ndani, Perez akubali mziki

Wachezaji nyota Eden Hazard, Paul Pogba, Mbappe na Sadio Mane wameendelea kuhusishwa na kujiunga na Real Madrid.

Ripoti kutoka kwa Mkurugenzi wa Los Blancos amezungumzia ‘plan’ A ya usajili ambapo miongoni mwa wachezaji waliyopo kwenye mstari wa mbele ni Hazard, Pogba, Mbappe na Mane hii ni kwa mujibu wa (El Confidencial)

Rais wa Madrid, Florentino Perez ameweka kitita cha fedha katika jitihada za kumuunga mkono Zinedine Zidane hali ambayo ni tofauti na hapo awali ambapo alikataa mpango wake na kuplekea Mfaransa huyo kutimka zake.  

Zizou aliondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu uliyopita lakini kwa sasa amerejea na kuwa tumaini jipya kwa Perez ndani ya Bernabeu.

Baada ya kupitia kipindi kigumu kwa kutolewa na Champions League na Copa del Rey huku ikishindwa kufanya vizuri LaLiga, Zidane amekuwa tumaini jipya.

Mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard akiwa ndiyo lengo la kwanza kusajiliwa chini ya Zidane.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amwahi kunukuliwa akieleza namna anavyo mkubali Zidane “Namheshimu sana Zidane, yeye ni ‘idol’ wangu namshukuru sana nimeanza kucheza mpira,” Hazard amekiambia kituo cha Tv cha Ubelji.

Madrid inaamini itaweza kukamilisha usajili wa Hazard, nyota na Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe.

Mbappe amejiunga na PSG akitokea AS Monaco na kufanikiwa kufanya vema kwenye michuano ya World Cup akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa.

Baada ya Zidane kuzungumza na Perez kama kunanafasi ya kumnasa Mbappe ili kuja kuisaidia Madrid, Zidane ambaye anatoka taifa moja na Mbappe amesema kuwa huwenda kuna kitu wanaweza kufanya.

Ni kama masihara hivi lakini ni ukweli kuwa Rais wa Madrid, Perez anavutiwa sana na kijana huyo anayekipiga PSG.

“Mmoja kati ya walionifanya niupende mpira wa miguu alikuwa Zidane, nimekuwa nikimfuatilia sana,” amesema Mbappe mwaka 2017.

Na Paul Pogba anatamani kujiunga na Real tangu alipojiunga na Manchester United akitokea Juventus mwaka 2016 huku akihusishwa na Madrid hasa kutokana na uwepo wa Zidane.

“Sikuzote nasema kuwa Real Madrid ni klabu ya ndoto za wachezaji wote, ni moja kati ya timu kubwa duniani, Zidane yupo pale kama kocha, ni ndoto za kila mtoto au mchezaji,” amenukuliwa Poga akisema kwenye moja ya mahojiano yake.

Lakini pia Zidane anahitaji kumsajili nyota wa Liverpool, Sadio Mane na Marca, kazi kubwa aliyoonyesha Msenegal huyo kwenye mchezo wa fainali wa Champions League dhidi ya Real huko Kiev kunamfanya kumtaka kwa udi na uvumba.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW