Habari

Waziri Mwijage aanza kazi kwa kasi: Arejesha viwanda 10 serikalini

Serikali imefanikiwa kurejesha kwenye miliki yake viwanda 10 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji na kushindwa kuviendeleza kwa mujibu wa mikataba ya makabidhiano huku ikitoa muda wa uangalizi kwa viwanda vingine 28 vinavyosuasua hadi kufikia Agosti 22 mwaka huu viwe vimeainisha mpango kazi wa uzalishaji unaoeleweka la sivyo vitatwaliwa na kugawiwa kwa watu wengine wenye uwezo wa kuviendesha.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage

Akitaja viwanda vilivyorejeshwa serikalini, Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema ni viwanda vya Mbao Mkata, Korosho Lindi, Chuma Taifa Manawa Ginnery, Tembo cheap board na Mangula mekanical tools, vingine ni mgodi wa Pugu dabaga tea factory, Polysacks DSM na kiwanda cha nguo Kilimanjaro kilichopo Arusha huku akisema orodha hiyo sio ya mwisho kwani bado zoezi hilo linaendelea.

Zoezi la kubaini viwanda hivyo limefanywa na kamati maalum chini ya msajili wa hazina kwa kushirikiana na serikali za mikoa wizara husika na wizara za kisekta na mwanasheria mkuu wa serikali ambapo waziri Mwijage amebainisha kuwa pamoja na kutaifishwa kwa viwanda hivyo, tayari viwanda 11 vimeanza kufanya kazi kufuatia agizo la Mhe Rais John Pombe Magufuli alilotoa tarehe 22 june mwaka huu la kutaka viwanda vyote vianze uzalishaji.

SOMA ZAIDI Rais Magufuli aagiza waliobinafsishiwa viwanda kuvirejesha serikalini

Hata hivyo, Waziri Mwijage amewataka wananchi kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili viwe endelevu huku akiahidi kwa wawekezaji kuwa serikali itahakikisha kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika viwanda ili kuvutia wananchi wengi kuingia kwenye sekta hiyo.

Miaka ya nyuma serikali ilibinafsisha jumla ya viwanda 156 ambapo mpaka sasa viwanda vinavyofanya kazi ni 62 viwanda 28 vinasusua visivyofanyakazi kabisa 56 na viwanda 10 vikibinafsishwa kwa kuuza mali moja moja.

Chanzo:ITV Tanzania

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents