AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Zinedine Zidane anukia kutua Chelsea, vikao vizito vyaendelea, kipigo cha 6 – 0 kutoka kwa Man City kumng’oa Sarri

Imeripotiwa kuwa miamba ya soka ya Uingereza klabu ya Chelsea ipo mbioni kutafuta saini ya aliyekuwa kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ili kuchukua mikoba ya Maurizio Sarri.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 46, Zidane amekuwa nje ya kazi yake kwa muda kidogo tangu kuachana na Real baada ya kuipatia mataji matatu mfululizo ya Champions League.

Sarri amekuwa kwenye wakati mgumu tangu alipopokea kichapo cha mabao 6 – 0 kutoka kwa Manchester City wiki iliyopita huku wakimpendekeza, Zidane kuchukua nafasi yake.

Taarifa kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa wiki hii kumekuwa na vikao ambavyo vikiendelea baina ya klabu hiyo na watu wa karibu wa Zidane ili kuhakikisha swala hilo linatimia.

Kutua kwa legendari huyo wa Ufaransa ambaye amewahi kutwaa kombe la dunia akiwa na Les Bleus,kutamfanya nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard kuongeza kandarasi mpya ya kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo vya Stamford Brige.

Image result for sarri

Hata hivyo Chelsea huwenda ikakumbana na vikwazo kutoka Manchester United ambao bado wapo mbioni kuhitaji huduma ya Zidane atakayechukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer ambaye alirithi mikoba ya Jose Mourinho aliyetimuliwa kazi katikati ya mwezi Desemba.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW