Burudani

Mrisho Mpoto kuzunguka Afrika na Ulaya kwaajili ya michezo ya majukwaani

Msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto anaondoka nchini Jumatano hii kuelekea Uganda kujiandaa kwaajili ya ziara ya michezo ya majukwaa katika nchi mbalimbali barani Afrika na Ulaya.

10784977_377486682408288_610215379_n

Mpoto ameiambia Bongo5 kuwa safari hiyo itamfanya aendelee kuitangaza Tanzania katika mataifa mbalimbali duniani.

“Mimi nitakuwa moja kati ya watu watakaofanya Theatre Play katika nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya,” amesema. “Mimi nilichaguliwa nikiwa kama aritst niliyetoka Tanzania lakini story ilikuwa imeandikwa kutoka Nigeria na Ken Saro-wiwa, ni story inaitwa Africa Kills Her Sun. Kwahiyo tukachukuliwa na hiyo taasisi tukachanganywa na wasanii mbalimbali wa East Africa na tukafanya kazi nchini Kenya. Baada ya hapo tukapata huo mchezo ambao kwa Tanzania ni mimi nikaungana na watu watatu tukaifanya hiyo project. Tuliwai perform kule Marekani na nchi nyingi nyingi za Ulaya. Sasa mwaka huu ndo tunaanza hiyo tour ambayo tutaifanya katika mataifa mbalimbali. Kikubwa ni kuitangaza Tanzania yetu pamoja na utamaduni wa kitanzania.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents