Burudani

Ferooz afungua mgahawa wenye thamani ya shilingi milioni 30

Msanii wa muziki aliyewahi kutamba na kibao cha ‘Starehe’ Ferooz amesema ametiza ndoto yake ya miaka miwili ya kufungua mgahawa uliogharimu shilingi milioni 30.

feroo

Ferooz ameiambia 255 ya XXL kuwa mgahawa huo uitwao Hollywood Cafe, utakuwa ukitoa huduma ya za chakula pamoja na vinywaji.

“Hii ni biashara ambayo tuliipanga kuifanya kama miaka miwili iliyopita,” alisema. “Mpaka sasa hivi ni kama milioni 30 hivi kwa sababu pale tulilipia kama miaka miwili iliyopita ndo tukaanza kufanya ukarabati nini, vitu vya hapa na pal. Yaani sio kitu cha kufanya kwa muda mmoja. Tulitaka kutengeneza kitu fulani classic hata kuweka heshima ya msanii na heshima ya Bongo Flava.”

“Ni pale Dar free market nimefungua na tunatarajia kufanya grand open. Nipo mimi na wife wangu mtarajiwa ambaye ndo tuko pamoja kwenye biashara. Kwahiyio Jumatano tunafanya grand open. Ni restaurant ambayo itakuwa na vyakula na vinywaji na vitu kama hivyo. Huu mgahawa unaitwa Hollywood Café kwa sababu mwanzo tulikuwa na biashara inaitwa Hollywood Fashion lakini sasa hivi tumeamua kuuita Hollyhood Café.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents