Burudani

Rapper Nelly akamatwa na madawa ya kulevya na silaha

Rapper wa ‘Hot In Herre’, Nelly yupo kwenye maji ya moto.

179363501_nelly_640 (1)

Rapper huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye jina lake halisi ni Cornell Haynes, alikamatwa Jumamosi iliyopita akiwa na madawa ya kulevya, bangi na dawa za paraphernalia, kwa mujibu wa polisi wa barabarani wa jimbo la Tennessee.

Wakili wa Nelly, Scott Rosenblum alidai kuwa mteja wake pia alikutwa na dawa za MDMA zinazojulikana pia kwa jina la Molly.

Katika msako kwenye gari lake la ziara, polisi walikuta pia mawe yaliyogundulika kuwa na madawa ya methamphetamine na bunduki kadhaa.

Watu sita walikamatwa kwenye gari hilo akiwemo Nelly.

Rapper huyo ametoka kwa dhamana ya $10,000 na anatarajiwa kupanda kizimbani June 19.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents