Michezo

Paul Scholes: Manchester United haikuwa na mpangilio wowote

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Paul Scholes amsema kuwa timu yake hiyo ya zamani ilikuwa haifai na haikuwa na mpangilio wowote ilipofungwa 2-0 na Liverpool kulingana na Paul Scholes ambaye alikuwa kiungo wa kati wa timu hiyo.

32140EA700000578-3486622-Former_Manchester_United_midfielder_Paul_Scholes_was_less_than_p-a-50_1457649122016

Magoli ya Liverpool yalifungwa na Daniel Sturridge na Firmino na kudidimiza matumaini ya Manchester United huku David De gea akizuia mashambulio mengi ya Liverpool.

Scholes aliambia BT Sport kwamba klabu hiyo ya Old Trafford huwa na viwango fulani lakini kufikia sasa imefeli kuafikia viwango hivyo.

Aliongezea:Liverpool ilikuwa na mpango wa kucheza,Lakini United hawakuwa na mpango wowote.

Awamu ya pili ya mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa Old Trafford Alhamisi ijayo.

”Manchester United inafaa kuwania ligi ya Uingereza na kombe la vilabu bingwa”,alisema Scholes.

Wametumia pauni milioni 300 na bado wako katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi.

Wameshushwa hadi katika ligi ya Europa baada ya kushindwa katika kombe la vilabu bingwa.

Wanafaa kushindana na Barcelona,Real Madrid na Bayern.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents