Michezo

Rais wa Fifa aungana na FUFA kuomboleza kifo cha kipa wa Uganda

Rais wa shirikisho soka duniani (FIFA), Giovanni Infantino ametuma salamu za rambi rambi kwa shirikisho la soka Uganda (FUFA) kwa ajili ya kifo cha Abel Dhaira.

Dhaira jenezani

Infantino alituma ujumbe huo uliopokelewa na Rais wa FUFA, Moses Magogo wakati wa kusanyiko la ibada ya mazishi zilizofanyika mapema hii leo katika kanisa la All Saints Cathedral lililopo Nakasero jijini Kampala .

Aidha, Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Issa Hayattou alituma salamu zake wiki iliyopita ambapo pia aliridhia ombi la FUFA la kutaka kuwepo kwa dakika moja ya ukimya kabla ya kupigwa kwa mechi ya kufuzu michuano ya AFCON kati ya Uganda na Burkina Faso.

dhaira-3

Ibada hiyo ya kumsalia marehemu Dhaira ilihudhuriwa na waziri wa michezo nchini Uganda, , Charles Bakabulindi, kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin Sredojevic (Micho), wachezaji wote wa timu ya taifa ya Uganda, Meya wa jiji la Kampala, Elias Lukwago na wanafamilia ndugu jamaa na marafiki.

Hata hivyo, mashabiki wa soka watapata nafasi ya kuuwaga kwa mara ya mwisho mwili wa marehemu, Abel Dhaira kwenye uwanja wa Nakivubo kabla safirishwa kuelekea Jinja, nyumbani kwa baba yake kwa ajili ya mazishi siku ya kesho (Jumatano).

Dhaira ambaye aliwahi kuchezea timu ya Taifa ya Uganda, alifariki siku ya Jumapili pasaka nchini Iceland kwa maradhi ya kansa ya utumbo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents