Burudani
Nandy amchukua Mr Blue kwenye remix ya Nagusa Gusa
Nandy ameamua kumchukua Mr Blue kwaajili ya remix ya ngoma yake, Nagusa Gusa.
Amesema ameamua kuja remix ili kutafuta ladha tofauti. Akiongea kwenye kipindi cha Extra Fleva cha Uplands Fm – Njombe kinachoendeshwa na Ergon Elly,Nandy alisema awali kwenye wimbo huo alitakiwa kumshirikisha msanii lakini kwa kuhohofia maneno ya watu kuwa amebebwa, ilibidi autoe akiwa mwenyewe.
Ameongeza kuwa remix imechangamka zaidi na baada ya Fiesta watashoot video yake.
Msikilize zaidi hapo chini.