Biilioni 5 kwa atakayefichua wauaji wa kimbari

Balozi Maluum wa Marekani (Uhalifu wa Kivita), Clint Williamson ameahidi na kusisitiza kuwa ile kutoa tuzo ya dola milioni 5 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh 5 bilioni za Tanzania) iko pale pale kwa watakaotoa taarifa

Clint Williamson


 


Balozi Maluum wa Marekani (Uhalifu wa Kivita), Clint Williamson ameahidi na kusisitiza kuwa ile kutoa tuzo ya dola milioni 5 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh 5 bilioni za Tanzania) iko pale pale kwa watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita ambao wako mafichoni kwa hivi sasa.



Tuzo inayojulikana kama US Reward for Justice Programme, ikiwa inalenga kutoa motisha kwa watu wengi zaidi kushiriki katika juhudi za kuwasaka watuhumiwa maarufu wa mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita ambao hadi sasa hawajakamatwa na wanaendelea kusakwa.



Aidha Balozi huyo alitoa mfano wa mtuhumiwa maarufu ambaye anasadikiwa kuwa alikuwa mfadhili wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 ambaye hadi sasa hajakamatwa kutokana na kuwa mafichoni.



Wengine ni wahalifu wawili wa kivita waliokuwa viongozi katika vita vya Bosnia ambao wanatuhumiwa kwa ukatili mkubwa waliofanya katika vita vilivyoteketeza maelfu ya watu katika Yogoslavia ya zamani.



“Wapo baadhi ya watuhumiwa ambao wanatakiwa kushtakiwa katika utaratibu wa kimataifa. Hatutafurahi kuona watu kama hao wanashtakiwa katika utaratibu wa mahakama za nchi zao,” alisema wakati katika mahojiano na Shirika la Habari la Hirondelle.



Hivi sasa Balozi huyo yupo katika ziara rasmi ya kutembelea Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) na kwamba alifanya baadhi ya mikutano na viongozi waandamizi wa Mahakama hiyo akiwemo Rais wake, Jaji Dennis Byron kuhusu watuhumiwa ambao bado hawajatiwa mbaroni.



Alipoulizwa iwapo kama suala la kuwashtaki watuhumiwa wa mauaji ya kimbari toka Kundi la Waasi la zamani la RPF pia lilijadiliwa, Balozi William alisema kuwa majadiliano yao yalikuwa ni ya kijumla tu bila kutaja kesi maalum.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents