Michezo

Jina lamponza mtangazaji wa michezo nchini Marekani

Mtangazaji wa michezo wa shirika la utangazaji la ESPN, Robert Lee ametolewa katika ratiba ya kutangaza mchezo wa vyuo vikuu kati ya Virginia dhidi ya William vyote vikiwa vinapatikana katika mji wa Charlottesville.


Robert Lee ametolewa katika ratiba ya kutangaza mchezo huo kutokana na jina lake kufanana na lile la shujaa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Jenerali Robert E Lee.

Shirika hilo limesema Lee sasa atatangaza mtanange baina ya Youngstown State dhidi ya Pittsburgh inayotarajiwa kupigwa Septemba 2 mwaka huu.

Waandamanaji mbalimbali walijitokeza mwezi huu kupinga kuondolewa kwa sanamu ya Jenerali Lee wanajeshi wa majimbo ya kusini yaliyokuwa yanapigania kuendelezwa kwa utumwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents