Michezo

Yanga SC yalicharukia gazeti la michezo nchini kwa kosa hili

Klabu  ya soka ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wake wa makundi nchini umelaani vikali kitendo cha muandishi wa habari wa gazeti la Mwanaspoti kuandika mashabiki wa Simba SC kupitia mitandao ya kijamii wamempa pole Kocha Lwandamina kwa msiba wa mwanae pamoja na kumpatia ubani wa Tsh. 3 milioni badala ya Yanga SC.

 

UPOTOSHWAJI WA MAKUSUDI ULIOFANYWA NA GAZETI LA MWANASPOTI LA LEO JUMATATU 15/01/2018

KATIKA HABARI ILIYOPO UKURASA WA PILI IKIWA IMEANDIKWA NA MWANDISHI KHATIMU NAHEKA.
Aya 3 za Mwisho ameandika “Mashabiki mbalimbali wa Simba kupitia mitandao ya kijamii. siku ya Jumamosi Wamempa pole Kocha Lwandamina kwa msiba wa mwanae pamoja na kumpatia Ubani wa Tsh. 3 milioni.”
KITU AMBACHO SI KWELI.
Huku ni kuwakosea heshima mashabiki wa Yanga ambao kwa umoja wao ndiyo waliompa kocha wa timu yao pendwa Ubani huo, kupitia michango ya group za WhatsApp.

Nichukue nafasi hii kuwaomba wanayanga wote kulaani vikali upotoshwaji huu wa makusudi wenye lengo la kuchafua heshima ya klabu,wanachama na mashabiki wa Yanga.
By Robert Kasela
Mwenyekiti
Umoja wa Group za Yanga.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents