Michezo

Alan Shearer amtaja mchezaji anayestahili kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka EPL

Mchezaji wa zamani wa Newcastle United, Alan Shearer amemtaja mchezaji anayestahili kushinda tuzo hiyo. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache kupita tangu Chama cha Wachezaji wa kulipwa nchini England (PFA) kutangaza majina ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya EPL msimu huu.

Shearer amemtaja mchezaji huyo ambaye anastahili kuchukua uzo hiyo ni Mohamed Salah ambaye mpaka sasa amefunga magoli 30 katika ligi kuu ya Uingereza.

Akiongea na The Sun, Alan Shearer amesema Salah anastahili kushinda tuzo hiyokuliko Kevin De Bruyne wa Manchester City. “Hakuna mtu angeweza kutabiri Salah angekuwa kama taa nyekundu kama alivyokuwa Liverpool ilimsajili msimu wa majira ya joto,” amesema Shearer.

“Kwa kweli, kulikuwa na sababu moja au mbili zilizotolewa wakati Liverpool walipolipa paundi milioni 34.3 kwa ajili yake, hata kama hiyo ilikuwa zaidi kwa sababu ya muda wake Chelsea ulivyopotea. Lakini kwa sasa atapata kura yangu kwa Mchezaji wa Mwaka,” ameongeza.

“But with what Salah did in those two ties, scoring his goals and pulling his team through to the semi-final, he would now be my pick. De Bruyne has also been magnificent and he was again on Saturday against Tottenham. But I realise how difficult it is to score goals and that’s why I would give it to Salah, who now has 40 in all competitions for Liverpool,” amesisitiza.

Wachezaji wengine ambao wametajwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Harry Kane (Tottenham Hotspur), David De Gea (Manchester United), David Silva na Leroy Sane (Manchester City).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents