Michezo

UEFA yamtangaza Cristiano Ronaldo kuwa mshindi bao bora la msimu 2017/18

Chama cha soka barani Ulaya (UEFA) kimemtangaza mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo kuwa mshindi wa goli bora la msimu wa mwaka 2017/18.

Ronaldo ametangazwa mshindi baada ya bao lake safi maarufu kama (bicycle kick goal) alilofunga kwenye mchezo wa tarehe 03 mwezi Aprili mwaka 2018 dhidi ya Juventus hatua ya robo fainali michuano ya UEFA Champions League.

Nyota huyo ambaye kwa sasa anaitumikia Juventus ambayo ndiyo aliifunga bao hilo ametangazwa mshindi baada ya kupata karibia kura 200,000 kati ya 346,915 zilizopigwa.

Mchezaji huyo raia wa Ureno amepokea kijiti kutoka kwa Mario Mandžukić ambaye alichukua tuzo hiyo msimu uliyopita ilhali hasimu wake Lionel Messi akitwaa mara mbili mfululizo msimu wa mwaka 2014/15 na 2015/16.

Nafasi ya pili imekwenda kwa Dimitri Payet akiitumikia Marseille iliyoibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5-2 akipachika bao kwenye mchezo huo dhidi ya RB Leipzig akipata kura 35,558.

Na nafasi ya tatu ikienda kwa Eva Navarro bao alilofunga dhidi ya Ujerumani akiitumikia timu yake ya taifa ya Hispania ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 0 – 2 akipata kura 23,315 mchezo wa fainali michuano ya UEFA European Women’s Under-17 Championship.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents