Burudani

Trey Songz kuburuzwa mahakamani kwa kushindwa kutoa hela za matibabu

Msanii wa muziki wa R’n’B nchini Marekani, Trey Songz amefunguliwa upya mashtaka na mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Andrea Buera ambaye awali alimshtaki kwa kosa la kumpiga na kumchania nguo hadharani kwenye mchezo wa kikapu wa NBA All-Star mwezi Februari mwaka huu.

Image result for trey songz
Trey Songz

Mrembo Buero amefungua mashtaka hayo upya ambapo awali kesi hiyo ilitupiliwa mbali baada ya mahakama mjini Los Angeles kukosa ushahidi juu ya tukio hilo.

Kwa sasa mrembo huyo amefungua mashtaka mapya akitaka alipwe mkwanja wa kufidia matibabu na gharama za kupoteza muda wa kutibiwa na vitu alivyopoteza siku ya tukio.

Image result for andrea buera and trey songz
Andrea Buero

Hata hivyo, nyaraka mpya za mrembo Buero zinaeleza kuwa Trey Songz alimshambulia Buero baada ya kumuona akiongea na mwanaume mwingine nje ya ukumbi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents