BurudaniDiamond Platnumz

Kipindi Cha Mkasi Kuja Na Mabadiliko Baada ya Kutimiza Mwaka Mmoja.

Salama Jabir
Kwa wale ambao mlikuwa hamjui, kipindi mahiri cha mahojiano katika masuala mbali mbali ya kijamii, “MKASI ambacho kinarushwa katika luninga ya EATV kila siku za Jumatatu majira ya saa tatu usiku, kimetimiza mwaka mmoja tangu kuonekana kwa mara ya kwanza Tarehe 14 Mwezi wa kumi na moja Mwaka 2012, na kwamba kinatarajiwa kuboreshwa zaidi.
Kipindi hicho ambacho kinaendeshwa na mtangazaji wa zamani wa EATV, Salama Jabir kinachotumia mfumo wa Barbershop interview, kitakuja na mabadiliko ambayo watanzania watajulishwa katika siku za usoni. Tukizungumza na mmoja wa wamiliki wa kipindi hicho AY alisema ili kuboresha na kutowaboa watazamaji, wanafanyia kazi ubunifu mpya ambao hata hivyo hakutaka kuuweka wazi. “Ni kweli tutakuja na mabadiliko lakini kwa sasa siwezi kuweka wazi ni nini hasa tutakacholeta katika kipindi hicho”.
Kipindi hicho kimejizolea umaarufu wa kutosha kutokana na namna kinavyopangiliwa katika kuchagua mgeni, mada, na maswali ya kizushi ambayo mara nyingi mtangazaji Salama Jabir huuliza papo kwa papo.
Baadhi ya watu ambao wameshawahi kuhojiwa katika kipindi hicho ni pamoja na Marehemu Steven Kanumba, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bwana Lawrence Masha, Januari Makamba, Hashim Thabeet, Aden Rage, Credo Mwaipopo, Diamond, Ali Choki, Nakaaya sumari, Ray, Dully Sykes na Steve Nyerere.
Bongo5 inapenda kuwapa pongezi waandaaji, waongozaji na watangazaji wa kipindi hicho. Big up guys kwa kuliendeleza libeneke.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents