Habari

Kubenea afikishwa Mahakamani kwa kuingiza fedha za Kigeni nchini bila kutoa tamko

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, kupitia Chama cha ACT-Wazalendo Saed Kubenea, anatarajiwa kufikishwa Mahakamani muda wowote kwa tuhuma za kuingiza nchini fedha za kigeni bila kutoa tamko kinyume na Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha Mpakani.

Saed Kubenea

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP Biswalo Mganga hii leo Septemba 7, 2020.

“Mnamo tarehe 5/9/2020, Jeshi la Polisi Tanzania lilimkamata Saed Kubenea akiwa katika gari la abiria lenye namba ya usajili T. 645 DKR akitokea kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Namanga akielekea Arusha mjini”, imeeleza taarifa ya DPP Biswalo.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, “Mara baada ya upekuzi, mtuhumiwa huyo alikutwa, pamoja na vitu vingine, Dola za Marekani 8,000, Shilingi za Kenya Laki Nne Tisini na Moja Elfu Mia Saba, Shilingi za Kitanzania Elfu Sabini na Moja, tiketi ya basi la Super Couch lenye namba ya usajili KCP 4230 ya tarehe 05/09/2020 kutoka Nairobi, Kenya kwenda Namanga”.

“‘Memorandum of Understanding’ kati ya Hali-Halisi (Tanzania) na Buni Media Limited (Kenya), Risiti ya malipo ya hoteli iitwayo After 40 Hotels Limited iliyopo Nairobi, Kenya yenye jina la Kubenea, Saed Ahmed kama mgeni kuanzia tarehe 3/9/2020 hadi 5/9/2020 na Pasi yake ya kusafiria (Passport)”, Imeeleza taarifa hiyo.

Endelea kusoma taarifa hapa chini,

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents