Burudani

Kala Jeremiah kuja na ‘Karibu Dar’ aliomshirikisha Ben Pol

Baada ya mwaka jana kufanya vizuri na Dear God, rapper Kala Jeremiah anatarajia kuachia ngoma mpya iitwayo ‘Karibu Dar’ ambayo inaelezea maisha ya vijana wa kitanzania wanaokimbilia maisha ya Dar na kuziacha fursa zilizopo katika katika maeneo yao.

311249_439383286099032_153871850_n

Katika ngoma hiyo, Kala amemshirikisha Ben Pol. Akiongea na Bongo5 Kala amesema:

Wimbo wangu mpya unaitwa karibu Dar nimefanya na Ben Pol wimbo huu umefanyika chini ya studio za Smart Music chini ya producer Mbezi. Kwanini karibu Dar? Mwaka 2011 mwishoni nilianza project ambayo nilikuwa mimi na Roma ambayo tulikuwa tunawafuata watu na kuongea, hasa hasa watu wa vijijini tulifanikiwa na kuanza na kanda ya ziwa ambako tulifanikiwa kukutana na wavuvi, wachimbaji wadogodogo wa madini lakini pia tulikutana na watu ambao wanaishi pembeni ya migodi. Kwahiyo lengo lilikuwa nikujua maisha halisi ya mtanzania na kujua umaskini wa mtanzania. Tuna mambo mengi sana ya kufanya na hiyo project, na project bado inaendelea na tulisimamisha kwasababu tulikuwa na mambo mengine ya kufanya lakini project inaendelea na itaendelea kwa muda mrefu kidogo ni project ya miaka mingi kidogo kwahiyo nadhani project hii itakuja na majibu mengi sana.

Wakati nafanya project hii nikagundua kuwa pia vijana wengi wa kitanzania wanaamini Dar es Salaam ndio sehemu pekee ya kijana wa kitanzania kutoka kimaisha kwamba wanaamini ili utoke kimaisha lazima upite Dar es salaam au lazima ufike Dar es saalam. Hii kwangu ikawa kama kikwazo nilivyo rudi Dar es salaam kufanya research maisha halisi ya mtu anayetoka huko na kuja huku na kujaribu kutafuta maisha nilivyovigundua humu na maisha ya watu wanao kuja kwa staili hiyo au maisha halisi watu ambao wa staili hiyo au maisha halisi ya watu wa kawaida wa Dar es salaam. Kwasababu Dar es Salaam kuna maisha ya aina mbil. Kuna maisha ya juu sana na kuna maisha ya chini yani kuna sehemu maji hayatoki mwezi mzima na kuna sehemu maji yanatoka mwaka mzima.

Kwaiyo ujaribu kuona hiyo tofauti. Nimejaribu kuongea ukweli na uhalisia na video tayari imeshafanyika chini ya Next level chini ya mtayarishaji Adam Juma, kwahiyo kila kitu kiko sawa, watu wasubiri muda siyo mrefu ngoma itakuwa hewani. Naomba watanzania waipokee kama walivyo pokea ngoma yangu nyingine. Niseme kwa ujumla kwamba namshukuru Mungu kwa kuniongoza vitu vya kufanya kwasababu napofanya vitu kama hicho najisikia vizuri kwasababu namwelewesha mtu,na mwelimisha mtu kwamba najua siku moja ama baada ya miaka fulani atakuwa mtu fulani. Kwahiyo vijana au watu ambao wapo kwenye mikoa mbalimbali washikilie fursa walizokuwa nazo na wafanye kazi na fursa walizo nazo pale walipo na waamini wakifanya vizuri watatoka. Ukitaka kuja Dar, sikiliza Karibu Dar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents