Burudani

Chiku: MC Mkali wa Kike Bongo!

Mara ya kwanza naisikia sauti ya Chiku Keto na kusikilizia style yake ilikua kwenye bss ya kwanza kufanyika bongo. Nafsi yangu ilinambia wazi kwamba bongo hip hop imepata kichwa now kwa upande wa akina dada. Nakumbuka kina dada kibao walikuwa wakali kwenye game mfano Rah-P, Sister-P, Ghetto Queen, Zay B na wengine kibao, lakini ni wazi kwamba ujio wa Chiku Keto ni wa aina yake, kishindo heavy kupitia songi lake la “muda umefika” akimshirikisha Lameck Ditto.

Dada huyu ambaye kwa sasa ndio kiongozi mtendaji wa kundi la “la familia”amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweka sawa issue za muziki kwa upande wake japokuwa mimi binafsi sikuridhika na ujio wake wa pili katika wimbo wake”nateseka” aliomshirikisha Chidi Benz.

“Naona kama amejilazimisha sana kushusha tempo yake ili aweze kuimba wimbo huo ambao mimi huuchukulia kama blues…..anyway naamini atakuwa anajipanga kuja katika style ileeeeeeeee ambayo wengi tulimkubali” alisema mdau mmoja wa hip hop.

Hivi karibuni bongo5 imesikia habari kuwa Chiku yuko mbioni kufanya track mpya na video.

Tukae mkao wa kula!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents