BurudaniDiamond Platnumz

Diamond Aungana na Sharobaro

Nassib Abdul a.k.a. Diamond na wenzake waliyo chini ya lebo ya Sharobaro wameamua kuunda umoja wenye jina hilo ili kwenda sambamba na makundi mengine katika game ya muziki ya kizazi kipya.

Kiongozi wa Sharobaro, Rahim Ramadhani a.k.a. Bob Junior amesikika akisema kwamba wameamua kufanya kazi pamoja ili kujiongezea nguvu badala ya kila msanii kusimama kivyake.

Jumla wapo wasanii nane, na baada ya kuungana wameanza kutengeneza ngoma mpya ya kutambulisha Sharobaro yenye jina la Jiongezee.

Umoja huo unaundwa na Diamond, Richard Mavoko, Ude Ude, Man Moe, Alinda, Nyoka, Malilo na Bob Junior.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents